OFISI
YA RAIS – TAMISEMI
HALMASHAURI
YA WILAYA YA NAMTUMBO
SHULE YA
SEKONDARI NASULI,
S.L.P21,
NAMTUMBO.
ANWANI YA SIMU
10/06/2017.
SIMU Na: 0754404552
0786251224
KUMB.NA:
MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI
______________________________________
S.L.P ____________________
__________________________
YAH:MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA
SEKONDARI NASULI ILIYOPO HALMASHAURI YA NAMTUMBO, MKOA WA RUVUMA MWAKA 2017.
1.Nafurahi kukutaarifu kuwa mwanao amechaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano katika shule hii mwaka 2017. Shule ya Sekondari
Nasuli ipo umbali wa Kilometa 65 Mashariki mwa mji mkuu wa Mkoa wa Ruvuma (Songea) na Kilometa
185 Magharibi mwa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Usafiri wa basi kutoka mjini Songea unapatikana
katika Kituo cha Mabasi cha Msamala, nauli ni Shillingi 2,500/=. Ukifika Namtumbo telemka katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha
Namtumbo na Shule yetu ipo upande wa pili wa barabara kuu.
Muhula
wa masomo unaanza tarehe 17/07/2017 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 01/08/2017.
Mwanafunzi atakayechelewa kuripoti kwa tarehe hizo,
nafasi yake atapewa mwanafunzi mwingine.
2.1 Sare ya
Shule
a) Sare
ya shule hii ni sketi ya rangi ya kijani kibichi yenye marinda kuzunguka kiuno
chote yenye marinda kuzunguka kiuno chote yenye urefu wa sentimeta 15 toka
unyayoni. (Sketi fupi hazikubaliki) Sketi ziwe mbili au zaidi.
b) Shati
nyeupe mikono mifupi (Mashati mawili au zaidi).
c) Viatu
vyeusi vya kufunga na kamba vyenye visigino vifupi.
d) Sare
ya michezo kwa shule hii ni track suit nyeusi.
e) Sweta
rangi ya kijani kibichi.
f) Nguo
za kushindia (Shamba dress) ni gauni rangi ya damu ya mzee, mshono ni solo.
Gauni liwe refu sentimeta 15 toka unyayoni.
g) Rangi
ya hijab ifanane na sare ya shule.
h) Soksi
jozi mbili nyeupe.
2.2 Ada na
Michango
a) Ada
ya shule ni shilingi 70,000/= kwa
mwaka. Unatakiwa kulipa shilingi 35,000/=
kwa muhula. Fedha hizo zilipwe kwenye Akaunti ya Shule namba 62401100009 katika Benki ya NMB (Tafadhali
andika jina la mwanafunzi kwenye pay in slip. Pay in slip hiyo iletwe shuleni
siku atakayoripoti mwanafunzi).
b)
Michango
inayotakiwa kulipwa na kila mzazi ni:-
i.
Shilingi 15,000/= kwa ajili ya ukarabati wa samani.
ii.
Shilingi 6000/= kwa ajili ya kitambulisho na picha.
iii.
Shilingi 20,000/= kwa ajili ya taaluma.
iv.
Shilingi 30,000/= kwa ajili ya kuwalipa wapishi, walinzi na vibarua wengine.
v.
Shilingi 2000/= nembo ya shule.
vi.
Shilingi 10,000/= , kwa ajili ya
huduma ya kwanza Tsh 5,000/= na Bima ya Afya (CHF)Tshs.5,000/=.
vii.
Shilingi 20,000/= Mitihani ya Kujipima “Mock”.
viii.
Fedha ya tahadhari Tshs 5000/= (haitarejeshwa).
Michango hii pia ilipwe katika Akaunti ya Shule
iliyotajwa hapo juu.
NB: Jumla ya ada na michango kwa mwaka kwa
mwanafunzi ni Shilingi 178,000/=.
c)
Mahitaji
muhimu ambayo mwanafunzi anapaswa kuleta shuleni ni:-
i.
Ream ya karatasi moja A4 kwa mwaka.
ii.
Vitabu vya masomo ya tahasusi husika .
iii.
Dissecting kit kwa wanafunzi wa Biolojia.
iv.
Scientific calculator.
v.
Godoro kwa wanafunzi wa bweni.
vi.
Mashuka (pea mbili, rangi ya blue bahari
na pink), blanketi, mto,foronya .
vii.
Vyombo vya chakula (sahani, bakuli,
kikombe na kijiko).
viii.
Ndoo mbili ndogo zenye mifuniko.
ix.
Kwanja moja, jembe moja, mifagio ya
ndani na nje.
3.
MAKOSA YATAKAYOSABABISHA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE.
i.
Wizi
ii.
Kutohudhuria masomo kwa zaidi ya siku 90
bila taarifa/utoro
iii.
Kugoma na kuhamasisha mgomo
iv.
Kutoa lugha chafu kwa wanafunzi wenzake,
walimu/ walezi na jamii kwa ujumla.
v.
Kupigana mwanafunzi kwa mwanafunzi,
kumpiga mwalimu au na mtu yeyote Yule
vi.
Kusuka nywele kwa mtindo usiokubalika.
Wanafunzi wote wanatakiwa kuwa na nywele fupi wakati wote wawapo shuleni au
kusuka kwa mtindo wa ususi uliokubalika na uongozi wa shule
vii.
Kufuga ndevu
viii.
Ulevi au unywaji wa pombe na matumizi ya
madawa ya kulevya
ix.
Uvutaji wa sigara
x.
Uasherati, uhusiano wa jinsia moja ,
kuoa au kuolewa
xi.
Kupata ujauzito au kutoa mimba
xii.
Kushiriki matendo ya uhalifu, siasa na
matendo yoyote yale yanayovunja sheria za nchi
xiii.
Kutembelea majumba ya starehe na nyumba
za kulala wageni
xiv.
Kumiliki , kukutwa au kutumia simu ya
mkononi katika mazingira ya shule
xv.
Kudharau Bendera ya Taifa
xvi.
Kufanya jaribio lolote la kujiua, au
kutishia kujiua kama kunywa sumu n.k
xvii.
Uharibifu wa mali ya Umma kwa makusudi.
4. Viambatanisho
na fomu muhimu
a) Fomu
ya uchunguzi wa afya (Medical examination form) ambayo itajazwa na Mganga Mkuu
wa hospitali ya Serikali
b) Fomu
ya maelezo binafsi kuhusu historia ya mwanafunzi, mkataba wa kutoshiriki katika
mgomo, fujo na makosa ya jinai
c) Fomu
ya mzazi kukiri kukubaliana na sheria, kanuni, kulipa ada, michango na
maelekezo mengine yatakayotolewa na shule
d) Picha
nne (4) za wazazi na ndugu wa karibu wa mwanafunzi wanaoweza kumtembelea
mwanafunzi shuleni pamoja na namba zao za simu
5. Tafadhari soma kwa makini maelezo , maagizo haya
na kuyatekeleza kikamilifu
KARIBU SANA KATIKA SHULE HII
_________________________________
AMOS
C. MAPUNDA
MKUU
WA SHULE
Kiambata “A”
FOMU YA
KUKUBALI KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI NASULI.
A. Sehemu ya Mwanafunzi
Mimi ………………………………………………………………………….
Ninakubali nafasi niliyopewa kuingia Kidato cha Tano kwa tahasusi ya
…………………. mwaka ………………katika Shule ya
Sekondari ya Nasuli na nitafika shuleni bila kuchelewa. Ninaahidi kwamba nitatii
na kuzingatia sheria zote za shule na za nchi. Ninaahidi kutoshiriki katika
mgomo, fujo na makosa ya jinai.
Nitakuwa mwanafunzi mwenye bidii katika
masomo na kazi za Elimu ya kujitegemea.
Anuani yangu ya kudumu ni
……………………………………………………………………………….
……………………………………………
……………………………………………
…………………………………………..
Sahihi………………………………….. Tarehe ………………………
B. Sehemu ya Mzazi/Mlezi
Mimi …………………………………………………ninakubali mtoto
wangu ……………………………………………………
Kuchukua nafasi kuingia Nasuli shule ya
sekondari kidato cha tano tahasusi ya ………………….... mwaka …………………..
Ninaahidi kumpatia mahitaji yote ya
shule kama ilivyo katika maagizo ya kujiunga na shule. Pia nakiri kukubaliana na sheria, kanuni za
shule pamoja na kulipa ada, michango na maelekezo mengine yatakayotolewa na
shule.
Ninakuhakikishia kuwa nitashirikiana na
shule wakati wote kuona kuwa mwanangu anatekeleza wajibu wake kwa shule na
Taifa.
Anuani yangu ya kudumu ni:-
……………………………………………………
……………………………………………………
Iwapo nitapata uhamisho au kubadili makazi,
ni lazima nitaijulisha shule kwa maandishi.
Sahihi………………………………….. Tarehe ………………………
Kiambata “B”
TAARIFA BINAFSI YA MWANAFUNZI
1. Jina lako kamili lilivyotumika kidato
cha nne…………………………………….
Dini yako/dhehebu
…………………………………………………………………………
2. Jina kamili la baba mzazi/mlezi
…………………………………………………………
Kazi yake
………………………………………………………………………………………
Anwani kamili ya baba mzazi/mlezi
…………………………………………………….
Na. yake ya simu ya mkononi
……………………………..
Na. yake ya simu ya mezani
…………………………….....
Mahali anakoishi baba mzazi/mlezi: Mkoa
…………………… Wilaya …………
Tarafa …………………………………………. Kata ……… Kijiji/Mtaa…………………………………………………………………………
3. Jina kamili la mama mzazi/mlezi
………………………………………………………..
Kazi yake
……………………………………………………………………………………….
Anwani kamili ya mama mzazi/mlezi
……………………………………………………………………………………….
Na. yake ya simu ya mkononi
……………………………….
Na. yake ya simu mezani ……………………………………..
Mahali anakoishi mama mzazi/mlezi: Mkoa
…………………. Wilaya …………
Tarafa ……………………………………Kata …………………….
Kijiji /Mtaa…………..
4. Majina ya watu watatu wanaoruhusiwa
kumtembelea/kumchukua mtoto wako
Na.
|
Jina
lake
|
Uhusiano
|
Mahali
anakoishi
|
Anwani
na namba yake ya simu
|
||||
01
|
|
|
|
|
||||
02
|
|
|
|
|
||||
03
|
|
|
|
|
||||
5. shule nilizosoma msingi hadi kidato cha nne
Na.
|
Jina la shule
|
Darasa/
kidato
|
Kuanzia
mwaka hadi mwaka
|
Mkoa
|
Wilaya
|
Kijiji/Kata
|
01
|
|
|
|
|
|
|
02
|
|
|
|
|
|
|
03
|
|
|
|
|
|
|
04
|
|
|
|
|
|
|
05
|
|
|
|
|
|
|
Namba yangu ya mtihani
wa kidato cha nne …………………………..
Kiambata
“C”
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S
OFFICE
REGIONAL
ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENTS
NAMTUMBO
DISTRICT COUNCIL
NASULI SECONDARY SCHOOL,
P.O BOX 21,
NAMTUMBO.
10.06.2017.
DISTRICT MEDICAL OFFICER
P.O.BOX …………..
…………………………
Dear Sir/Madam.
Re : A
REQUEST FOR MEDICAL EXAMINATION.
Please
examine Mr./Miss ……………………………… as to his/her physical and mental fitness for
admission as a Form Five Student at Nasuli Secondary School in the year 2017.
Yours sincerely,
……………………………..
AMOS C.
MAPUNDA
HEAD OF
SCHOOL
__________________________________________________________________
The Headmaster,
I have examine Mr./Miss ………………………………as
shown below and consider that he/she is physically and mentally fit/unfit for
admission to pursue a full time secondary education.
1. Vision with/without glasses. Right
……………………… left ……………
2. Blood pressure ……………………………………
Haemoglobin ……………
3. Hearing …………………………………………….
4. Urine (a) Albumen ……………………………. (b)
Sugar ……………………
5. (a) Venerial diseases …………………………..(b)
Bilharzia ………………
6. Pregnancy ………………………………………………………………………
7. Neurosis ……………………………………………………………………
8. Is there any abnormality of:-
(a) The heart …………………………………. (b) Lungs
……………………
(c) The spleen …………………………………
9. Are there any serious diseases e.g.
leprosy, epilepsy, asthma, diabetes etc.
……………………………………………………………………………………….
Any comments ………………………………………………………………………
………………….. …………………………………….
Date
Signature of Medical Officer
Station:……………
................
Designation …………………………