Wednesday, 29 March 2017

DHANA YA UHAKIKI WA FASIHI



Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.

Maana ya Uhakiki

Dhana ya Uhakiki
Fafanua dhana ya uhakiki
Uhakiki ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Hii ina maana kwamba uhakiki wa kazi za fasihi hautoki katika ombwe, kuna kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza kufanya uhakiki, na hii ndio sababu kuna nadharia kadha wa kadha za uhakiki wa kazi za kifaishi. AU kwa lugha rahisi tunaweza kusema, uhakiki ni uchambuzi wa kina wa kazi za fasihi kama vile riwaya, tamthiliya na mashairi kwa lengo la kufafanua vipengele vya fani na maudhui.

Misingi ya Uhakiki
Kwa ujumla mhakiki wa kazi za fasihi anapofanya uhakiki wa kazi za kifasihi, huwa analenga vipengele viwili. Pengine analenga kuhakiki fani ya kazi husika au maudhui ya kazi hiyo na wakati mwingine vyote viwili. Kwa hiyo kupitia vipengele hivi ndipo atachambua vitu vingi kama vile ujumbe, falsafa, matumizi ya lugha, dhamira, mandhari na kadhalika.
Kuhakiki Fani
Katika utunzi wa kazi za kifasihi, Fani hutumika kama nyezo ya kuwasilisha mawazo ya mwandishi kwa njia ya kisanaa zaidi. Fani ni mbinu anayoitumia mwandshi ili kufikisha ujumbe kwa watu aliowakusudia.
Vipengele vya fani ni pamoja na wahusika, mandhari, lugha, muundo na mtindo.
Mtindo
Mtindo ni mbinu ya kipekee kifani na kimaudhui, zinazotofautisha msanii mmoja na mwingine. Kwa mfano, namna msanii anavyotumia lugha, anavyoteua msamiati, namna anavyosimulia hadithi yake (anaweza kutumia nafsi ya kwanza, ya pili au ya tatu). Kwa mfano katika riwaya ya “Barua Ndefu kama hii” iliyoandikwa na Mariama Ba ametumia mtindo wa barua ya kirafiki kuanzia mwanzo hadi mwisho, hii pia inaonesha mtindo wake wa kipekee.
Muundo
Muundo ni mpangilio wa kiufundi anaoutumia mwandishi katika kupangilia kazi yake. mpangilio na mtiririko wa kazi ya fasihi, kwa upande wa visa na mtukio.
Kuna aina mbili za kupangilia matukio
  1. Msago; hii ni namana ya moja kwa moja ya kusimulia matukio, yaani kuanzia tukio la kwanza hadi la mwisho kwa namna yalivyotukia. Huu ni muundo wa moja kwa moja.
  2. Urejeshi; huu ni usimuliaji wa kurukaruka hatua, yaani msimuliaji anaweza kuanzia katikati, akaja mwisho na kumalizia na mwanzo
Wahusika
Wahusika; ni watu au viumbe ambavyo mwandishi wa fasihi huwatumia ili kufanikisha ujumbe kwa jamii husika. Katika kazi ya fasihi mwandishi huwagawa wahusika katika makundi mawili yaani wahusika wakuu na wahusika wadogo.
Wahusika wakuu ni wale ambao wanajitokeza kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa kazi ya fasihi. Wahusika wadogo ni wale wote ambao wanajitokeza sehemu mbalimbali katika kazi ya fasihi kwa mfano, mwanzoni mwa kitabu hadi mwishoni mwa kitabu.
Wahusika hawa wawe ni wakuu au wadogo wanaweza kugawanyika katika makundi yafuatayo:
  1. Mhusika mviringo ni mhusika ambaye anabadilika kitabia na kimawazo kulingana na hali halisi ya maisha. Kwa mfano wanaweza kuanza kama watu wema lakini hali ya maisha ikawabadilisha na kuwa watu wabaya au wanaweza kuanza kama watu wabaya na hali ya maisha ikawabadilisha na kuwa watu wema.
  2. Mhusika bapa ni mhusika ambaye habadiliki kulingana na hali halisi ya maisha. Mfano; kama ni mwema basi atakuwa mwema kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho na kama ni mbaya basi atakuwa mbaya kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho.
  3. Mhusika shinda yuko katikikati ya mhusika papa na mviringo. Huongozwa na matendo ya hao wahusika wawili. Hajitokezi na msimamo wake imara.
Mandhari
Mandhari; hii ni sehemu ambayo matukio ya hadithi au masimulizi hutokea. Mandhari huweza kuwa halisi kama vile baharini, njiani, msituni, kijijini, mijini au ya kufikirika kama vile kuzimu, mbinguni, peponi n.k.
Lugha
Lugha ndio nyenzo kubwa ya msanii katika kazi za fasihi, miongoni mwa vipengele vya lugha ni tamathali za semi pamoja na semi.
Fani za Lugha
  • Tanakali za Sauti:Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika.
  • Tashbiha:Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; ‘kama’, ‘mithili ya’, ‘sawa na’, ‘ja’. mfano, Mwembamba kama sindano.
  • Tashihisi: Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Mfano, "Sungura aliposhindwa, akasema sizitaki hizi mbichi".
  • Takriri:Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Mfano, alikimbia, alikimbia, alikimbia hadi akashika nafasi ya kwanza.
  • Ukinzani: Ukinzani ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana.
  • Sitiari: Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo ‘ni’ ama ‘kuwa’. Mfano; Maisha ni mlima, juma ni mwamba.
  • Taswira: Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.
  • Taashira: Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa.
  • Jazanda: Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi.
  • Majazi: Majazi ni pale tabia za wahusika zinapoambatana na majina yao halisi.
  • Lakabu: Ni mbinu ya mhusika kupewa/kubandikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake. (Nickname)
  • Chuku: Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu, kutilia Chumvi.
Semi
Ni fungu la maneno linapotumika kutoa maana nyingine, badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi:
  • Nahau – ni usemi unaotumia maneno ya kawaida kwa lengo la kufikisha maana iliyotofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo. Nahu huwa na vitenzi.
  • Misemo – ni semi fupifupi ambazo hutumiwa mara kwa mara kwa lengo la kuleta maana maalumu. Misemo haina vitenzi.
Maswali ya Balagha
Tashititi au maswali ya balagha ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo hayahitaji jibu.
Uzungumzi Nafsiya
Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.
Ritifaa
Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo) kana kwamba yuko pamoja nawe.
Kuchanganya Ndimi
Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili. Mfano, "alisimama kwanza kwa muda, before he went aliniambia nisimwambie mtu yeyote yule, you know!"
Kuhamisha Ndimi
Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu. Mfano: Kazi hii ni ngumu sana, sitaweza kuifanya. People are trying to convince me to stay here but I think I can't, I must go!
Methali
Methali ni misemo ya hekima yenye maana iliyofumbwa. Mhusika, mwandishi wa fasihi anaweza kutumia methali kupitisha ujumbe.
Mbinu nyingine za Kisanaa
  • Kinaya; Kinaya ni mambo katika sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira.
  • Kejeli; Kejeli ni mbinu ya sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani.
  • Taharuki; Taharuki ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kufanya hadhira na/au wahusika wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kuilazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali.
  • Sadfa; Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa, japo havikuwa vimepangiwa.
  • Kisengere Nyuma; Mwandishi ‘hurudi nyuma’ na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa akisimulia. Aidha, mwandishi hubadilisha wakati wa masimulizi na kuwa wakati wa kisa hicho. Hutumika sana kuonyesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutupatia msingi wa jinsi mambo yalivyoanza. Mbinu Rejeshi.
  • Kisengere Mbele; Mwandishi anapobadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia lugha isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri. Utabiri.
Kuhakiki Maudhui
Maudhui; Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusanii kazi fulani ya kifasihi. Vipengele vya maudhui ni pamoja na dhamira, migogoro, falsafa ujumbe na msimamo.
  1. Dhamira; hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Dhamira ni sehemu tu ya maudhui na aghalabu dhamira kuu ndio hujenga kiini cha kazi ya fasihi. Dhamira zimegawanyika katika makundi mawili, kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo.
  2. Migogoro; hii ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi za fasihi. Migogoro inaweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka yao, au hata katika nyadhifa mbalimbali. Vilevile migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, mogogoro ya nafsi, na migogoro ya kisiasa ambayo hujitokeza katika mitazamo tofauti kulingana na mtiririko wa visa na matukio yanavyopangwa na mwandishi.
  3. Ujumbe; mwandishi anapoandika kazi yake huwa na ujumbe ambao hutaka uifikie jamii aliyoikusudia. Ujumbe katika kazi fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi. Katika kazi ya fasihi dhamira kuu hubeba ujumbe wa msingi na dhamira ndogondogo hubeba ujumbe ambao husaidia kuujenga au kuupa uzito zaidi ujumbe wa msingi.
  4. Msimamo; katika kazi ya fasihi, mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Msimamo ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili huweza kukataliwa na wengi lakini akalishikilia tu. Msimamo ndio huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Kwa mfano, katika tamthilia ya “Pesa zako zinanuka” mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi kwani amejadili matatizo yanayochangia kukwama kwa ujenzi wa jamii mpya.
  5. Falsafa ni mawazo ya busara yenye kutawaliwa na misingi mahususi juu ya asili na maana ya ulimwengu na maisha ya mwanadamu. Ni msimamo wa msanii katika maisha juu ya utatuzi wa matatizo katika jamii. Falsafa ya mwandishi inaweza kujulikana kwa kusoma kazi zake zaidi ya moja.
  6. Mtazamo ni hisia au uelewa wa mwandishi juu ya jambo fulani. Kwa mfano anaweza kutazama jambo fulani kwa mtazamo wa kidini, au anaweza kutazama jambo fulani kwa mtazamo wa kisiasa au kisayansi.
  7. Mafunzo; ni mawazo ya kuelimisha yanayopatikana katika dhamira mbalimbali za kazi ya fasihi.
Kufaulu na Kutofaulu kwa mwandishi
Kufaulu au kutofaulu kwa mwandishi kunategemea jinsi alivyoweka uwiano mzuri kati ya fani na maudhui kwa namna ambavyo inaleta uhalisia. Mfano, endapo msanii atakuwa na mhusika Mkongo lakini akawa anazungumza kiswahili kilichojaa misemo na nahau alafu kimenyooka kama mtu wa pwani itakuwa vigumu kusema amefaulu kwani hakuna uwiano mzuri kati ya mhusika mwenyewe na lugha anayoitumia. Kiswahili cha Kongo ni tofauti kabisa na kiswahili kinachozungumzwa na watu wa pwani (Tanzania).

UTUNGAJI WA  KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Kazi za fasihi andishi ni sanaa, yaani zinahitaji ubunifu wa mwandishi ili ziwe katika mwonekanao huo wa kisanaa. Fasihi andishi hutumia lugha na wala sio lugha tu bali lugha ya kisanaa, kama tulivyokwishaona katika mada zilizotangulia kwamba lugha ni kipengele muhimu sana katika fasihi. Ili kazi ya kifasihi ya msanii husika iwe nzuri na ya kuvutia, masanii hana budi kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kutumia lugha.
Msanii awe na uwezo wa kupangilia maneno, kuteua maneno katika hali ya ujumi lakini pia yakiwa yamebeba ujumbe unaoigusa hadhira yake. Kwa maana hii mwandshi wa kazi za kifasihi, iwe riwaya au tamthilia ni lazima azingatie sana lugha, kwani lugha ndio nyenzo kuu ya usanaa wa fasihi kwa ujumla.
Kuna hatua kadhaa za kuzingatia wakati wa kuandika kazi ya kisanaa, hatua hizo ni kama zifuatazo:
  • Kuwa na kisa/wazo unalotaka kuliandikia:Katika jamii kuna mambo mengi sana yanayotendeka, msanii anaweza kupata wazo la kiubunifu kutokana na mambo hayo yanayotendeka katika jamii. Kama tujuavyo fasihi andishi kazi yake ni kuonesha yale yanayotendeka katika jamii, kwa hiyo msanii anaweza kutumia fursa hiyo ili kuweka wazi mambo yanayoendelea katika jamii. Kwa mfano mwandishi naweza kutunga kazi ya kibunifu kuhusu, ufisadi, umasikini, mapenzi, ndoa, maisha yake mwenyewe, ushirikina, jambo lolote analoliamini katika maisha (falsafa yake). Kwa hiyo hatua ya kwanza kwa msanii kabala ya kuandika ni kuelewa vizuri jambo analotaka kuandikia. Pia katika hatua hii msanii anaweza kubuni jina la hadithi yake, pia hii inaweza kumsaidia katika upangaji wa visa na matukio ya hadithi yake.
  • Kuchagua umbo la kazi ya fasihi: Msanii akishapata wazo la kuandika, sasa inambidi achague jinsi atakavyoliwasilisha wazo lake hilo. Yaani anaweza kuchagua endapo aandike hadithi fupi, riwaya au tamthiliya, au ushairi au utenzi. Sasa uchaguzi wa umbo la kazi ya fasihi unategemeana na uwezo wa msanii katika tanzu hizo, kuna mwingine anapenda tamthiliya lakini kuandika riwaya hawezi, kuna mwingine anaona kuandika ushairi ni rahisi na kuna mwingine hawezi. Kwa hiyo ubunifu wa msanii utadhihirika katika utanzu ule anaoumudu vizuri zaidi.
  • Kubaini hadhira: Mwandishi kujua yule anayemwandikia ni suala la msingi sana. Hadhira ipo ya watu wa aina mbalimbali, watoto, watu wazima, wasomi, wenye elimu ndogo, wakulima, wanasiasa n.k. Sasa mwandishi akishabaini hadhira anayoindikia itamsaidia kuteua lugha ya kuandikia, kwa mfano kama ni watoto, hatutegemei mwandishi kutumia lugha ngumu, misemo na nahau nyingi.
  • Kubuni wahusika na mandhari: Mwandshi baada ya kujua kazi yake inahusu nini sasa inambidi abuni wahusika wa hadithi yake. Wahusika wanaweza kuwa ni watu, wanyama, mimea, mazimwi, malaika n.k. Pia ni lazima abaini mazingira ambamo visa vyote vya hadithi na matukio yatakapofanyika. Mandhari yanaweza kuwa baharini, kijijini, mjini, mbinguni, kuzimu n.k
  • Kupanga msuko wa visa na matukio:Msuko wa visa na matukio ni muhimu sana katika usimulizi wa hadithi. Sasa kama mwandishi amaeamua kuwasilisha kazi yake kwa njia ama ya hadithi fupi au riwaya au tamthiliya ni vema ajue namna visa na matukio vitakavyopangwa. Katika kufanya hivi maswali yafuatayo ni muongozo mzuri katika kupangilia ploti: Hadithi yangu itaanzaje? Mgogoro utaanzaje? Ni kati ya nani na nani? Je, kilele cha mgogoro ni nini? Je, ni mhusika mkuu kubakwa na kuambukizwa VVU? Hadithi yangu inaishaje? Je mhusika mkuu ashindwe? Atorokee nje ya nchi? Afungwe? Abadilike Au maadui ndio wafungwe au wafe? Au wabadilike?
  • Kuanza kuandika: Sasa baada ya kupitia hatua hizo zote, mwandishi sasa anaweza kuanza kuandika. Mchakato wa kuandika hua ni mrefu na mwandishi anaweza kujikuta anafuta mara nyingi kile alichokiandika, hii ni kutokana na kwamba mambo mengi ya kuandika huwa yanakuja wakati mwandishi ameanza kuandika kazi husika. Hata hvyo sio vibaya kufanya hivi, hii pia inasaidi kuwa na zao bora la fasihi.
Utungaji wa hadithi
Hadithi ni masimulizi ya kubuni yaliyoandikwa kinathari inaweza kuwa na wahusika wengi, matukio mengi na mandhari mapana (inategemena na aina ya hadithi, iwapo ni hadithi fupi wahusika wake huwa ni wachache na pia matukio ni machache, mandhari yake pia ni finyu). Kuna aina zifuatazo za hadithi kulingana na kigezo cha urefu au maudhui. Kwa kigezo cha urefu kuna Hadithi Fupi na Riwaya. Kutokana na maudhui kuna Riwaya Dhati na Riwaya Pendwa.
Riwaya dhati ni zile zinazozungumzia masuala muhimu ya kijamii, kama vile uonevu wa tabaka la chini, rushwa, uongozi mbovu n.k
Riwaya pendwa ni hadithi zenye lengo la kuburudisha, kutokana na usimuliaji wake uliojaa taharuki na fantasia. Mambo yanayosimuliwa katika riwaya hizi ni yale yanayogusa hisia za watu kwa urahisi kama vile mapenzi, mauaji, ujasusi n.k.
Mikondo ya uandishi wa hadithi
Mkondo wa hadithi ni mwelekeo ambao mwandishi anaufuata katika utunzi wa kazi yake. Mikondo ya utunzi wa hadithi ni pamoja na hii ifuatayo:
  1. Mkondo wa kiwasifu; mkondo huu huhusisha hadithi zote zinazosimulia maisha ya watu. Ni riwaya ambayo inasimulia maisha ya mtu toka alipozaliwa hadi wakati huo.
  2. Mkondo wa kitawasifu; hadithi zinazofuata mkundo huu ni zile zinazosimulia maisha ya mtu binafsi yaani mwandishi mwenyewe. Kwa mfano riwaya ya “maisha yangu baada ya Miaka hamsini”. (S.Robert)
  3. Mkondo wa kihistoria; hadithi katika mkondo huu zinahusu matukio ya kweli ya kihistoria yaliyotokea. Kwa mfano riwaya ya “Uhuru wa Watumwa”
  4. Mkondo wa kipelelezi; hizi ni hadithi zinazozungumzia upelelezi wa uhalifu fulani kama vile ujambazi, wizi, rushwa, mauaji n.k.
  5. Mkondo wa kimapenzi; katika mkondo huu zinaingia riwaya zote zinazozungumzia masuala ya mapenzi.
Utungaji wa hadithi fupi
Kama tulivyokwisha ona hapo nyuma sifa za hadithi fupi, basi katika utungaji wake mambo yafuatayo ni sharti yazingatiwe:
  1. Hadithi fupi inakuwa na mhusika mkuu mmoja ambaye anajitokeza sana kuliko wahusika wengine.
  2. Idadi ya wahusika ni ndogo ukilinganisha na wahusika wa kwenye riwaya.
  3. Mandhari ya hadithi fupi si mapana kama ilivyo katika riwaya
  4. Hadithi fupi inakuwa inaongelea dhamira kuu moja tu ambayo inaonekana toka mwanzo hadi mwisho wa hadithi.
Dhima ya Tamthiliya
Elezea dhima ya tamthiliya
Tamthiliya ni kazi ya fasihi iliyoandikwa kwa lengo la kuonyeshwa jukwaani, ambapo wahusika huzungumza na kutenda vitendo mbalimbali. Tamthiliya huigiza maisha ya kila siku.
Kwa kuwa tamthiliya imeandikwa kwa lengo la kuigizwa huwa imeandikwa na maelezo ya jukwaani, maelezo yanayoonesha nini kifanywe na nani na kwa namna gani. Tamthilya hugawanywa katika maonyesho kama ambavyo riwaya inavyogawanywa katika sura.
Tamthiliya imegawanyika katika aina zifuatazo:
  • Tanzia; ni aina ya tamthiliya ambapo mhusika mkuu/shujaa anapata anguko kubwa au kifo ambacho huwafanya hadhira kuwa na huzuni.
  • Ramsani tamthilia ambayo hulenga kufundisha kwa njia ya kuchekesha ili kuleta ujumbe mzito.
  • Vichekesho/Futuhi ni aina ya tamthiliya ambayo lengo lake kuu ni kuchekesha kwa kutumia mbinu ya kutia chumvi mambo, kudhihaki na kukejeli.
Utungaji wa Tamthiliya
Tunga tamthiliya
Katika utunzi wa tamthiliya kuna mambo kadhaa ya kuzingatia, mambo hayo ni kama yafuatayo:
  1. Chagua jambo unalotaka kuandikia
  2. Panga namna msuko wa visa na matukioa utakavyokuwa
  3. Buni wahusika wako kulingana na kile unachotaka kukiandika
  4. Chagua mandhari yanayofaa kulingana na visa vyako
  5. Tumia mtindo wa majibizano kati ya wahusika
  6. Gawa tamthiliya katika maonyesho
  7. Weka maelekezo ya jukwaa. Haya huelezea kile kinachotendeka kwa wakati ule. Maelezo ya jukwaa huwa katika maandishi ya italiki.
NA
MWL. VITUS J.M

ACTI0N VERBS IN ESSAY QUESTIONS



WORDS TO WATCH FOR IN ESSAY QUESTIONS

The following words are commonly found in essay questions. Understanding them is essential to success on such questions and examination in general. If you want to do well on essay tests, examination then study this page thoroughly. Know these words backward and forward. To heighten your awareness of them, underline the words when you see them in a test question.

Discuss: Consider and debate or argue about the pros and cons of an issue. Write about any conflict. Compare and contrast.
Enumerate: List several ideas, aspects, events, things, qualities, reasons, etc.
Evaluate: Give your opinion or cite the opinion of an expert. Include evidence to support the evaluation.
Explain: Make an idea clear. Show logically how a concept is developed. Give the reason for an event.
Illustrate: Give concrete examples.
Explain clearly by using comparisons or examples.
Interpret: Comment upon, give examples, describe relationships. Explain the meaning.
Describe, then evaluate.
Outline: Describe main ideas, characteristics, or events. (Does not necessarily mean to write a Roman Numeral/Letter outline.)
Prove(Verify): Support with facts (especially facts presented in class or in the text.)
State: Explain precisely.
Relate: Show the connections between ideas or events. Provide a larger context.
Summarize: Give a brief, condensed account. Include conclusions. Avoid unnecessary details.
Trace: Give the development, process or history of a thing, event or idea, especially by proceeding from the latest to the earliest evidence.
Define: Give the meaning; usually a
meaning specific to the course or subject.
Explain the exact meaning. Definitions are usually short.
Describe: Give a detailed account. Make a picture with words. List characteristics, qualities, and parts.
Analyze: Break into separate parts and discuss, examine, or interpret each part.
Contrast: Show differences. Set in opposition.
Compare: Examine two or more things.
Identify similarities and differences.
Criticize: Make judgments. Evaluate
Comparative worth. Criticism often involves
analysis.
Critical Analysis: Examine the topic or argument in terms of its strengths and weaknesses.
Diagram : Present a drawing, chart, plan or graphic representation in your answer.
Generally, you are also expected to label the diagram and a brief explanation or description may be required.
Comment: Make critical observations, even if they are fairly open-ended. Your texts, learning notes and discussion notes should provide sufficient guidelines and your own commonsense should prevail.
Account for: Give reasons for; explain.
Clarify: Identify the components of an issue/topic/problem/; make the meaning plain; remove misunderstandings.
Demonstrate: Show clearly by giving proof or evidence.
Justify: Show adequate grounds for decisions, a particular view or conclusions and answer main objections likely to be made to them.
Infer: Conclude something from facts or reasoning.

If any of these terms are still unclear to you, go to an unabridged dictionary. Thorough knowledge of these words helps you give the teacher (marker) what he/she is requesting.


PREPARED BY ;
SIR. J.M.VITUS
NASULI HIGH SCHOOL
DEPARTMENT OF ENGLISH
P.O. BOX 21 – NAMTUMBO.